Na Abel Paul,Jeshi la Polisi- Arusha

Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo nchini limesema kwa kipindi cha mwezi januari mpaka novemba mwaka huu limefanikiwa kukamata mifugo 8970 iliyokuwa imeibiwa maeneo mbalimbali hapa nchini kati ya mifugo 15065 maeneo mbali mbali hapa nchini.

Akitoa taarifa hiyo leo Disemba 18,2023 jijini Arusha Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini kamishna msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema Jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa elfu tatu miatano na ishirini ambapo amebainisha kuwa kesi za watuhumiwa hao zipo katika hatua mbalimbali za kiuchunguzi.

Aidha Kamanda Pasua ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na viongozi wa wafugaji kwa watu wachache wanaojihusisha na wizi wa mifugo Pamoja na utoroshaji wa mifugo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pia amewataka wafugaji kufuata taratibu za usafirishaji wa mifugo ili kuondokana na kero na mamlaka zinazohusika na ukaguzi wa mifugo hiyo pindi wanaposafirisha mifugo Kwenda maeneo tofauti tofauti na nje ya nchi.

By Jamhuri