Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewasili nchini Uturuki katika jiji la Instanbul, na kupokelewa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini humo Lt. Jen. Y. H. Mohamed, leo tarehe 03 Novemba, 2022.

Mhe. Dkt. Gwajima anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa tano wa masuala ya Wanawake na Haki utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia kesho Novemba 04-05, 2022 akiwa amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano huu utawezesha nchi washiriki uzoefu kutoka Mataifa mengine namna ya kushughulikia masuala ya haki na kanuni za kitamaduni kwa wanawake na kutoa fursa ya kuelezea uzoefu wa Tanzania katika kushughulikia haki za wanawake.

By Jamhuri