Monthly Archives: May 2019

Ufisadi, upendeleo CWT

Hali si shwari katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kwani wakubwa wa chama hicho kwa sasa wanatazamwa kwa jicho la kutiliwa shaka katika uadilifu wao baada ya kutumia ukabila, udugu na upendeleo wa kila aina kuendesha chama hicho, JAMHURI limebaini.  Tuhuma kadhaa zimeelekezwa kwa viongozi wa chama hicho, hasa Katibu Mkuu, Deus Seif. Miongoni mwa tuhuma hizo ni pamoja na ...

Read More »

Wajinga wengi hujulikana wanapojieleza

Utandawazi kama mfumo unaoongozwa na kuongoza uchumi wa soko, hutumia mawasiliano ya haraka na mepesi katika shughuli zake. Mfumo huu ulipoingia duniani, ulitishia na kuhatarisha uwepo wa mambo mengi tuliyoyazoea. Dhana ya utandawazi ni somo pana, pekee na mahususi kulizungumzia. Bila kulifahamu hilo kwa undani, ni rahisi kujiingiza katika ugomvi usiokwisha. Nachelea kusema, hata uchaguzi wa mada yenyewe kutumia neno ...

Read More »

Uhakiki wa uraia kero Ngara

Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Ngara mkoani Kagera imekuwa ikisababisha usumbufu kwa wananchi wilayani humo kuhusu uraia wa baadhi yao. Inaelezwa kuwa utaratibu wa maofisa Uhamiaji wilayani humo wa kuvizia mabasi na magari yanayofanya safari zake ndani ya wilaya na kuwakamata wasafiri wakihisiwa kuwa wahamiaji haramu, umekuwa na usumbufu mkubwa. JAMHURI limeelezwa kuwa ukaguzi huendeshwa kwa upendeleo, baadhi ya wasafiri ...

Read More »

Hifadhi ya Serengeti kuongezwa

Serikali inakusudia kuongeza ukubwa wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ameliambia Bunge kuwa wizara yake imetayarisha mapendekezo ya kubadili mpaka wa hifadhi hiyo. Kwa sasa ukubwa wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko katika mikoa ya Mara na Simiyu ni kilometa za mraba 14,763. Eneo linalokusudiwa kujumuishwa ni la Pori Tengefu la ...

Read More »

Zoezi la utayari katika afya EAC lipewe uzito

Mwezi ujao, kwa muda wa siku nne, kuanzia tarehe 11 hadi 14, Tanzania itashiriki zoezi la kupima utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani. Hali hiyo inatokana na nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kuwa katika hatari ya kuathirika na magonjwa ya mlipuko kama Homa ya Bonde la Ufa, Mafua Makali ...

Read More »

NINA NDOTO (19)

Uaminifu unalipa   Uaminifu ni tabia ya mtu  kuaminika. Kama watu hawakuamini si rahisi kutimiza ndoto yako. Uaminifu unalipa. Watu wakikuamini ni mojawapo ya hatua kubwa ya kuzifikia ndoto zako. Uaminifu hujengwa, lazima kuna mambo unatakiwa kuyafanya ili watu waweze kukuamini. Kuwa mwaminifu kwenye kazi unayoifanya, na kuwa mwaminifu kwenye majukumu yako ya kila siku. Uaminifu  huwafanya watu wafanye kazi ...

Read More »

Bandari: Taratibu za kusafirisha mzigo ng‘ambo

Kwa siku za karibuni yamekuwapo malalamiko yasiyo rasmi juu ya wateja kucheleweshewa mizigo inayosafirishwa nje ya nchi, hasa mizigo ya mazao yanayoharibika haraka (perishable goods) kama maparachichi. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeyaona malalamiko hayo kupitia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii. Kutokana na hali hiyo, Bandari imebaini kwamba, kwa kuwa Tanzania inaingia kwenye uchumi wa viwanda kwa kasi, ...

Read More »

Kumbukizi miaka 20 bila Mwalimu Nyerere

Tunakosea kuwasifu wakwapuzi   Mei 16, mwaka huu Chama cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) ambacho ni chama cha kitume ndani ya Kanisa Katoliki kiliandaa kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Dhamira ya kongamano ilikuwa Maendeleo Jumuishi na yenye kujali ustawi wa maisha ya wananchi. Mada mbalimbali zilijadiliwa. Mada mbalimbali zilitolewa. Mwenyekiti wa CPT, ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (15)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala yangu kwa kuahidi kuwa kuanzia makala ya leo nitaanza kuzungumzia kodi na tozo mbalimbali katika biashara. Katika makala hii ya Jinsi ya Kuanzisha Biashara Tanzania, kupitia vitabu na sheria mbalimbali nilizosoma, nimebaini kuwa kuna kodi za msingi saba na ushuru wa aina tatu. Kodi hizi ni kodi ya mapato (mtu binafsi), kodi ya makapuni, kodi ya ...

Read More »

Ndugu Rais uliliambia taifa vema Watanzania si wajinga

Ndugu Rais, kwa kuwapenda watu wako, uliwatahadharisha viongozi wao kuwa watambue ya kwamba Watanzania si wajinga. Wana uwezo wa ‘kuanalaizi’ na kuchambua mambo. Wakinyamazia jambo kubwa wajue mioyo yao haiko, ‘clear’. Ndugu yetu Harrison Mwakyembe Waziri wetu aliwahi kuliambia Bunge kuwa wananchi siyo mabwege. Kwa sasa katika mitandao ya kijamii na hasa kule bungeni kauli hizi zimetamalaki. Haijulikani wanaozitamka wanathibitisha ...

Read More »

Elimu nzuri inajenga fikra pevu

Hadi kesho katika taifa letu la Tanzania bado hatujakubaliana ni lugha gani tutumie katika kufundishia. Wengine wanapendekeza lugha ya kigeni, Kiingereza; na wengine wanaipendekeza lugha yetu ya Kiswahili. Hii ni kasoro kubwa! Wataalamu wa falsafa wanatuambia kwamba, fikra na mawazo ya mtu au jamii yamo katika lugha yake. Kwa hiyo kukomaa kwa fikra za mtu huenda sambamba na kukomaa kwa ...

Read More »

Kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa (3)

Ukitaka kufanikiwa jifanye kama mti. Refuka uwezavyo. Usiangalie miti mingine ilivyo mifupi ama ilivyo mirefu. Nisikilize kwa umakini hapa; Iko hivi, unalo jambo la kujifunza kutoka kwa walioshindwa kufanikiwa. Jifunze. Ukifahamu kilichowafanya wasifanikiwe, utajifunza namna ya kukabiliana nacho. Lakini pia, unalo jambo kubwa la kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa ili na wewe ufanikiwe kama wao au zaidi ya wao. Walioshindwa kufanikiwa ...

Read More »

Dk. Mengi alitoa mengi kwa ukarimu

Ukarimu ni mtihani. “Tunatengeneza riziki kwa kile tunachopata, lakini tunatengeneza maisha kwa kile tunachotoa,” alisema hayati Winston Churchill, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza. Ukarimu unapoongelewa kuna ambao wanajiweka upande wa kutoa na kuna ambao kila mara wanajiweka upande wa kupokea tu. Tuna watu duniani ambao ukarimu ni kama jina lao la katikati. Tanzania imempoteza siku za karibuni mtu wa ...

Read More »

Tupo hapa kwa kupuuza yanayosemwa

Tunaona juhudi za serikali za kuhamasisha mazingira mazuri ya biashara nchini. Wiki iliyopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameliambia Bunge kwamba serikali imo mbioni kufuta sheria zote zinazokwamisha biashara. Kauli ya waziri mkuu imetanguliwa na kauli nyingi kutoka kwa mawaziri wa biashara, uwekezaji na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hivi karibuni Kamishna Mkuu wa TRA ameonekana akipita huku na ...

Read More »

Afrika inahitaji dozi ya kujiamini

Mei, 1954 majeshi ya kikoloni ya Ufaransa yalipata pigo kali kutoka kwa wapiganaji wa Vietnam katika mapambano kwenye mji wa Dien Bien Phu. Yapo matukio ambayo hubadilisha mkondo wa historia ya ulimwengu na moja ya matukio haya ni mapambano haya ya Bien Dien Phu. Ni muhimu kukumbuka tukio hili kwa sababu ni somo la jinsi gani dhamira kubwa ya wanyonge ...

Read More »

Mpewa hapokonyeki ndiyo yake haki

Binadamu ni kiumbe mwenye uwezo wa kutambua mema na mabaya. Ana akili ya kufikiri na kutengeneza jambo au kitu. Lakini hughafilika kila mara, si mkamilifu. Ni mdhaifu katika matendo yake. Uwezo na akili alizonazo zinampa kiburi kuweza kutengeneza kitu akitakacho kwa faida yake na wenzake katika umoja wao. Uwezo na akili zake zinaishia katika kufikiri, kubuni na kutengeneza, si kuumba. ...

Read More »

Yah: Mhe. Rais, mamlaka ya watendaji wa kati ni kero

Salamu zangu nazielekeza kwa wasomaji wote wa waraka huu kila wiki. Najua kuwa mnaishi kwa matumaini sana, hasa katika kipindi hiki kigumu cha mpito, lakini kipindi hiki cha mpito ni kirefu kuliko wengi walivyotarajia. Najua dhamira ni nzuri na matokeo ni mazuri, lakini muda uliopangwa kuyasawazisha mambo haya haukutarajiwa uwe mrefu kiasi hicho, muwe wavumilivu, na siku zote wavumilivu hula ...

Read More »

TFF wanaiachaje Azam TV, RTD?

Ligi Kuu imekwisha kufikia tamati na Klabu ya Simba kutwaa ubingwa. Nitoe pongezi kwa Simba na uongozi wao kwa hatua hiyo kubwa. Lakini mbali na Simba, timu nyingine kadhaa zimeshiriki ligi hiyo kwa mafanikio hata kama si ya kiwango cha kutwaa ubingwa. Katika miaka isiyopungua 10 lilikuwa jambo gumu Watanzania kushuhudia ligi yao ikirushwa moja kwa moja kupitia kituo chochote ...

Read More »

Masele yametimia

Hatima ya Stephen Masele kuendelea au kutoendelea kuwa mbunge katika Bunge la Afrika (PAP) inajulikana wiki hii. Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekaliwa vibaya kisiasa, na aliyeshika mpini kwenye vita hiyo ni Spika Job Ndugai ambaye naye anatoka katika chama hicho. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa ni Makamu wa ...

Read More »

Mochwari ya Muhimbili mmmh!

Mpita Njia (MN) kwa umri alionao, anaona kuna haja ya kuyakaribia Maandiko Matakatifu na kuyaishi. Kwa umri wake amepitia mengi, lakini la hivi karibuni la kuingia katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili limemfanya azidi kuimarika kiimani. Ni kwa sababu hiyo MN ameanza kukariri baadhi ya vifungu. Baada ya kufika Muhimbili, akarejea maandiko katika Kitabu cha Ayubu ...

Read More »

Mazito aliyekwepeshwa kwa Magufuli

James Kunena aliyeporwa nafasi ya kuzawadiwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa mfanyakazi bora wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) alipigiwa kura na wenzake kwa kuwa alibuni vipuri vilivyotakiwa kuagizwa nje ya nchi. Hatua yake hiyo iliwashawishi wenzake kumchagua kuwa mfanyakazi bora lakini nafasi hiyo akapachikwa Focus Sahani ambaye hakustahili nafasi hiyo. Kutokana na hali hiyo, fukuto limezidi kuibuka miongoni ...

Read More »

Abambikiziwa uanachama mfuko wa jamii

Uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa miaka minne umeshindwa kulipa mafao ya kustaafu ya askari polisi aliyelitumikia jeshi hilo kwa miaka 33, kisa kabambikizwa uanachama katika mfuko mwingine. Thomas Njama, amestaafu Jeshi la Polisi mwaka 2015 akiwa Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu mkoani Arusha. Amesema PSPF wanatakiwa kumlipa kiinua mgongo cha Sh 47,162,022 na ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons