Monthly Archives: May 2019

Mwalimu Nyerere angekuwepo angesemaje?

Namshukuru Mungu nimeweza kuketi kuandika kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi hiki cha kumbukizi ya kuzaliwa kwake na kujiuliza swali ambalo bila shaka Watanzania wengine nao wamekuwa wakijiuliza: Mwalimu angekuwapo akaona utendaji wa Rais John Pombe Joseph Magufuli kwenye Awamu hii ya Tano, angesemaje? Watanzania tuliokuwapo Awamu ya Kwanza tulishuhudia uongozi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu ...

Read More »

Kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa

Kujiandaa ni kujiandaa kushinda na kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa. Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln (1809 – 1865) anasema: “Ukinipa saa sita ili niukate mti, nitatumia saa nne za awali kuliona shoka langu.” Hii ni busara inayoonyesha umuhimu wa kujiandaa. Dunia inamilikiwa na watu waliojiandaa kuimiliki. Huwezi kuimiliki dunia bila kujiandaa kuimiliki. Eleanor Roosevelt anasema: “Wakati ujao unamilikiwa na ...

Read More »

Unaitambua nguvu ya moja?

Moja ni mtihani. Kuna nguvu ya moja. Anayefunga goli ni mtu mmoja lakini timu nzima inafurahi. Lakini kwa upande mwingine kosa la mtu mmoja linachafua picha ya kundi zima, samaki mmoja akioza wote wameoza. Kuna nguvu ya moja. Kuna uwezekano mkubwa mtu kuidharau moja. Kumbuka mdharau mwiba mguu huota tende. Kuna nguvu ya moja. Okoa shilingi moja, shilingi moja itakuokoa. ...

Read More »

Nawapongeza Mpanju, DPP Biswalo

Miongoni mwa habari zilizopewa umuhimu katika toleo hili inahusu kuachiwa huru kwa mahabusu 201 waliokuwa katika magereza ya wilaya za Musoma, Tarime na Serengeti mkoani Mara. Kuachiwa kwao ni matokeo ya ziara ya ukaguzi ndani ya magereza hayo uliofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju; Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga na wadau ...

Read More »

Buriani Dk. Mengi

Kifo kimeumbwa, kifo ni faradhi. Kifo ni ufunguo wa kufunga uhai wa binadamu duniani na kufungua maisha ya milele ya binadamu huko ahera (mbinguni). Faradhi na ufunguo umemshukia ndugu yetu mpendwa, Dk. Reginald Abraham Mengi.  Reginald Mengi amefariki dunia. Ni usiku wa kuamkia Alhamisi wiki iliyopita katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu, Reginald alifariki dunia baada ya kuugua kwa ...

Read More »

Yah: Malipo ni hapa hapa duniani

Salamu ndugu zangu wote mliopata baraka ya kuishuhudia Pasaka. Sina hakika, lakini ni kweli kwamba wengi walipenda kufurahia ufufuko wake Yesu Kristo mwaka huu lakini haikuwa hivyo. Wapo ambao waliweka malengo ya miezi sita na mwaka, lakini mipango yao haikuwa na mkataba wa maisha au siha njema na mipango hiyo imevurugika. Vilevile nawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ...

Read More »

Ndugu Rais tupandishe madaraja

Ndugu Rais, Mei ‘Dei’ ya Mbeya imepita. Wanaotaka kujifunza wataisoma. Lo! Maandamano yalikuwa marefu! Lo, mabango yalikuwa mengi yale, lakini yote yalibeba ujumbe mmoja unaofanana. Ulisomeka: “Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana. Wakati wa mishahara na masilahi bora kwa wafanyakazi ni sasa.” Wafanyakazi walisisitiza nyongeza ya mishahara kwa nguvu zao zote kistaarabu. Tunasema kistaarabu kwa sababu katika nchi nyingine hali ...

Read More »

Hapatoshi Wydad vs Esperance

Hatimaye timu ya Esperance de Tunis ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco zimefanikiwa kufuzu katika hatua ya fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika (CAF Champions League). Esperance wameingia fainali baada ya kuwafunga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo goli 1-0 katika mechi ya raundi ya kwanza wakiwa uwanja wa nyumbani. Katika mchezo wa raundi ya pili wakiwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons