Na Mwandishi Wetu, JAMHURI MEDIA

Serikali imesema kuwa ina mpango wa kubadili jina la Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe na kuwa Nationa Instute for Mental Health

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika semina maalum iliyoandaliwa kwa Wabunge wa Bunge
la Tanzania kupata elimu ya masuala ya afya ya akili, Mfuko wa Taifa wa Bima yaAfya (NHIF) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).
“Tunakwenda kubadili jina la Hospitali ya Mirembe ili kujenga taswira mpya ndani ya jamii kwenye huduma zinazotolewa pale, mtu anaweza kwenda pale kutibiwa hata Malaria, lakini jamii inamuita ‘chizi’. Tunataka Mirembe iitwe National Instititue for Mental Health,” amesem
Ameongeza kuwa “Tunataka Hospitali ya Mirembe ifanye kampeni za hamasa na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya ya akili, matibabu, tafiti mbalimbali za masuala ya afya ya akili pamoja na kufanya mafunzo.

By Jamhuri