Na Mwamvua Mwinyi,JAMHURI MEDIA

Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemuhukumu Fadhili Hai,(58), Mkazi wa Kwa Mfipa  – Kibaha kifungo cha miaka 40, viboko 12 na kulipa fidia ya Sh milioni 04 baada ya kupatikana na hatia ya kuzini na binti yake na kumsababishia ujauzito.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 11/ 2023 imetolewa na Hakimu Mfawidhi Judith Lyimo wa mahakama ya Wilaya ya Kibaha wakati kesi ilipoitwa kwa ajili  ya kutolewa hukumu.

Akisoma hukumu hiyo ,Judith Lyimo ameeleza kuwa amemtia hatiani mshitakiwa huyo kwa Mujibu wa kifungu namba 158 (1) (b) na 2 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Imeelezwa , mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05/06/2021 majira ya saa 09:00 alasiri  huko Kwa mfipa, Wilaya ya Kibaha,Mkoa wa Pwani.

By Jamhuri