Na Catherine Sungura,JamhuriMedia,Kagera

Serikali inatarajia kujenga kituo maalumu cha matibabu ya magonjwa ya milipuko mkoani Kagera.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya kujionea utayari wa kukabiliana na tishio la Ebola mkoani hapa.

Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na jiografia ya mkoa huo,Serikali kupitia Wizara yake inaona ipo haja ya kujenga kituo kwenye ukanda huo ambao umezungukwa na nchi nyingi.

Amesema Jumuiya ya Kimatiafa inazitaka nchi kujiandaa na majanga hivyo lazima kuwekeza kwenye ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya milipuko.

Aidha,Waziri Ummy amewataka watumishi wa Afya kuwa tayari kuokoa maisha ya watu endapo atapatikana mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ebola.

“Watoa huduma za afya mnao wajibu wa kuokoa maisha ya wananchi hivyo wakati wa kuhudumia kumbukeni kuzingatia kukinga na kudhibiti maambukizi kwako mwenyewe” amesema.

Kwa upande mwinge Waziri huyo alizitaka kamati za usimamizi wa huduma za afya ngazi za Mikoa na Halmashauri kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wote kwenye maeneo yao.

Vilevile Waziri Ummy amewapongeza kamati hizo kwa utoaji wa huduma ila aliwataka kujiangalia upya na kuwataka wafanye kazi kwa usimamizi utakaoleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma.

Please follow and like us:
Pin Share