DAR ES SALAAM 

Na Mwalimu Paulo Mapunda

Hapo zamani Mungu alikwisha kufunua kupitia ndoto ya Nebukadreza, Mfalme wa Babeli (The King of the Ancient Mesopotamia) iliyotafsiriwa na Daniel, Nabii (Daniel 2:44, 45) kwamba utawala wa Mungu ndio utakaosimama mwisho baada ya mambo yote, hivyo ni vema kufanya uamuzi mapema ama kumtumikia shetani (utawala wa kitambo) au kumtumikia Mungu (utawala wa milele), uamuzi ni wako juu ya hatima ya maisha yako. 

Huu ni uamuzi wa kuwapo na kutokuwapo, chenye mwisho na kisicho na mwisho, shufwa na witiri au kifo dhidi ya uzima wa utukufu usio kufa.

Katika kuasisi mfumo mbadala tofauti na ule wa Mungu, shetani aliunda serikali yenye makao yake makuu kuzimu, huku ikisimamiwa duniani (mji mdogo) na mtu (aliyeasi kwa ushawishi wa shetani), kwahiyo vikundi kama Illuminate, Knight of Malta, Templer na vingine vingi, hizi ni idara muhimu katika utekelezaji wa ajenda za kishetani. 

Freemason ndilo kundi mama ambalo ndani yake tunakuta vikundi hivyo vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina jukumu na mpango kazi elekezi. 

Kuna vyenye jukumu la kushughulika na fedha, uchumi, utawala (kuweka na kuondoa serikali madarakani), dini, uaharibuji wa maadili, mambo ya kijeshi, ugaidi, uvunjifu wa ndoa na uharibuji wa mimba.  

Maandiko yanasema: “Mmesikia imenenwa mpende jirani yako na mchukie adui yako.” (huu ndio mfumo wa ulimwengu chini ya muasi shetani, chuki imetawala kila kona ya dunia hii, chuki ya mtu mmoja mmoja na chuki za kimfumo, chuki ndani ya familia, chuki katika taifa, chuki kati ya walionacho na wasionacho (matajiri na maskini), chuki kati ya wasomi na wasiosoma, chuki kati ya weusi na weupe, chuki kati ya wanaume na wanawake, chuki kati ya watawala na watawaliwa, chuki za kikabila, chuki za kidini, chuki za kimasilahi, chuki za kimaumbile (wenye makalio makubwa na wasio nayo), chuki kati ya walioolewa na wasioolewa, chuki kati ya wenye watoto na wasio nao, chuki kati ya waujuao mlo na wasioujua mlo, orodha ni ndefu sana.

Itoshe kusema kwamba chuki ni roho yenye nasaba na roho ya mauti, na zinatenda kazi pamoja, Yesu alilijua hilo akaasisi mfumo mbadala katika Mathayo 5:44: “Lakini mimi (Yesu) nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni, kwakuwa yeye huwanyeshea mvua wema na wabaya.” 

Yesu aliyasema hayo kwa kuwa alishaona mabadiliko tangu ule mfumo wa awali aliouasisi Mungu mwenyewe kupitia Adamu pale Edeni (mfumo wa “wawe na umoja kama sisi tulivyo,” Yohana 17) hadi mfumo wa utengano ambao shetani aliuleta kwa kumdanganya mtawala halali ambaye alikuwa ni mtu. 

Mfumo alioujenga shetani ulijikita katika kanuni ya ‘wagawe (ondoa umoja) ili upate kuwatawala (kwa msaada wa utengano wao) ‘Divide and Rule.’ 

Katika kusimika utawala wa umoja, Mungu aliasisi mfumo wa kiutawala wenye sura ya umbo mraba, ikimaanisha usawa wa watu wote kabla ya Mungu, hili linathibitishwa na kupasuka kwa pazia la hekalu lililokuwa likitenganisha patakatifu (watu wa kawaida) na patakatifu pa patakatifu (mahali alipokuwa akiingia mtu mmoja tu, kuhani wa zamu).

Musa alipokimbia kutoka Misri mara baada ya kumuua mtu (Mmisri), akiwa katika nchi ya wamidiani, kwa zaidi ya miaka 40, Mungu alimfundisha jinsi ya kutengeneza madhabahu ya umbo mraba (utawala, mfumo wa maisha, tamaduni, mfumo wa kifedha na kanuni zote za usawa wa kibinadamu), hata Nabii Eliya alitengeneza madhabahu ya umbo mraba iliyompa nguvu ya kuwashinda manabii wa Baal (Belzebul). 

Shetani aliubadili mfumo huu, na kuleta mfumo mbadala unaokweza watu wachache na kuwaacha wengi wasijue namna ya kuenenda. Hata Musa alipokuwa katika jumba la kifalme la Farao alifundishwa mfumo huu wa kiutawala na kanuni zake za kishetani.

Mfumo huo unawakilishwa na umbo Pembetatu (Triangle), kwamba wachache wanawatawala wengi kwa kanuni ya wastani ya Pareto au 80/20 ikimaanisha kuwa watawala ni wachache ilhali watawaliwa ni wengi, ni kama katika mpira wa miguu, wachezaji 11 kwa kila timu, idadi itengenezayo jumla ya wachezaji 22 uwanjani kwa timu mbili, huku mashabiki wakiwa mamilioni nje na ndani ya uwanja wapigao kelele kushangilia timu ikifanya vizuri na kulaumu pale ifanyapo vibaya wasijue hata timu imeandaliwaje au gharama kiasi gani zimetumika hadi kuifikisha timu uwanjani.

Kwa kutumia kanuni zake kuu tatu (Three Satanic Rules), shetani anaisukuma dunia kwenye ule mwisho (Dooms Day), kanuni hizo ni Mosi, wafanye waelewe kinyume (Let them understand vice versa) kama alivyoiasisi kupitia nyoka (Mwz. 3:1-7). Pili, kanuni ya namba, ishara na alama kutawala dunia (Let symbols, numbers and signs rules the world). Kwa mujibu wa kanuni hii, popote pale penye alama yao, basi wao ndio watawala. Tatu, kanuni ya Order out of chaos kwamba unaleta tatizo ukiwa na suluhisho tayari au unaleta machafuko ili kupitisha amri, muongozo au sheria fulani kwa masilahi ya waleta tatizo. Hii ndiyo kanuni iliyotumika kupitisha sheria ya ugaidi duniani kote mara baada ya tukio la kigaidi la Septemba, 11 kule Marekani.

Shetani katika kuonyesha upinzani kwa Mungu wa mbinguni, aliasisi amri zake tano (Five Satanic Laws, Isaya 14:13,14) zitoazo uelekeo wa matamanio ya utawala wake, amri hizo ni mbadala wa zile kumi za Mungu (Kutoka 20:2-17), kupitia amri zake hizo tano, akapanga majanga matano kabla ya kuunda mfumo mpya wa ulimwengu (New World Order, NWO). Majanga hayo matano yalipangwa kwa kutumia akili kubwa sana na kwa kuzingatia Nyakati (muda). 

Kwa shetani, matukio yanapokuwa katika mpangilio wa namba fulani kimfuatano, huwa anaamini kuwa yanakuwa na nguvu na muitikio mkubwa sana. Aliyetumika kuweka mpangilio huo wa namba ni Profesa wa Hisabati, Pythagoras. Kwa hiyo, shetani alimvuvia Pythagoras siri kubwa iliyo ndani ya namba na muda ili kutengeneza muundo mpya wa ulimwengu. Muasisi wa namba ni Mungu, shetani anaijua siri hii, hivyo anatumia kanuni ile ile ya Mungu kinyume. 

Wapythagoras walifahamu ukuu na utukufu wa namba, kwa wao 10 ni namba takatifu kwa kuwa ni jumla ya namba moja hadi nne (1+2+3+4=10), walikuwa na mchoro wa namba kumi (10). Ni Albert Pike aliyeweka mpangilio huo ndani ya Msahafu wa kimasonic (Morals and Dogma), Adam, W akaweka mpangilio huo ndani ya kitabu cha waliovuviwa (Codex Gigas or Satanic Bible). 

Mathalani, wakati wa uumbaji zilipita saa 144 hadi pale Mungu alipomuumba mtu (Adam) yaani siku ya sita. Kwa Wapaithagoras sita humaanisha mtu, haki ni namba kipeuo cha pili na ndoa ni namba tano. Ilipita miaka 300 tangu kuumbwa Adam hadi kuumbwa Hawa (kumbuka kuwa siku moja kwa Mungu, ni sawa na miaka 1,000 kwa binadamu). Zile zinazotajwa kama siku saba za uumbaji na mapumziko kwa Mungu ni sawa na miaka 7,000 kwa binadamu.

                                                                       Tuwasiliane: [email protected];  0755 671 071.   


Itaendelea…

By Jamhuri