Latest Posts
Rais Kagame si wa kumwamini sana
Makala iliyopita ya “JWTZ nginjangija Goma hadi Kigali’, imenifumbua macho. Nimepata simu nyingi na ujumbe wa maandishi usio idadi. Wapo waliotumia lugha kali, lakini wengi walikuwa waungwana. Hiyo ndiyo raha ya mijadala. Kuna wakati tunaweza kukubaliana kwenye baadhi ya mambo, na wakati mwingine tusikubaliane kwa hoja fulani fulani. Muhimu ni kujenga moyo wa uvumilivu na staha.
Sote tukiwa waoga nchi itayumba
Ni kosa kubwa kwa mtoto wa Kizanaki kumtamkia mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Hawa ni tofauti na makabila mengine, mathalani Wajita. Wao mtoto ana uhuru na haki ya kumtamkia mzazi au mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Wakati Mzanaki atapambana kumnasa vibao mtoto anayeamini kamtukana, mzazi wa Kijita atafanya juhudi za kupambana kwa hoja kumthibitishia mtoto yule kwamba yeye (mkubwa) si mwongo. Hizo ni tofauti za wazi kwa makabila hayo mawili.
Messi alipa faini ya kukwepa kodi
Nyota wa timu ya soka ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi pamoja na baba yake mzazi wamelipa euro milioni tano, sawa na dola milioni 6.6 za Marekani, baada ya kubainika na kosa la kukwepa kodi. Messi na mzazi wake huyo walidaiwa kukwepa kulipa kodi hiyo ya serikali kwa njia za ujanjaujanja.
Kambi ya upinzani walitoka na hoja zao
Wiki iliyopita, Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na vibweka na vimbwanga vingi vyenye kuacha kinywa wazi kwa mshangao na hamaki kwa mtu yeyote makini mwenye kuujali mustakabali mwema wa nchi yake.
Hata hivyo, pamoja na vibweka na vimbwanga vilivyotokea kwenye kikao hicho, ukweli unabaki kuwa kilikuwa kikao chenye moja ya miswada muhimu yenye kipekee unaokwenda kuweka jiwe jipya la msingi kwa Tanzania tunayoihitaji kuijenga kwa miaka 50, au hata 100 ijayo.
Hotuba iliyochafua hali ya hewa ndani ya Bunge
MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.
- Tanzania yapata fursa nyingine za ajira 4,500 nchini Qatar
- MBT yavuta umati Geita, Wizara ya Madini yafungua dirisha jipya la fursa kwa vjana na waawake
- Mhandisi Swedi awaagiza wachimbaji kuimarisha usalama migodini kukabiliana na El Nino
- Sakata la mgomo wa madereva, ACT Wazalendo wataka Waziri Katambi ajiuzulu
- Mashili atimiza ahadi, akabidhi msaada wa kichomeo taka na jenereta Chuo cha Uuguzi Nzega
Habari mpya
- Tanzania yapata fursa nyingine za ajira 4,500 nchini Qatar
- MBT yavuta umati Geita, Wizara ya Madini yafungua dirisha jipya la fursa kwa vjana na waawake
- Mhandisi Swedi awaagiza wachimbaji kuimarisha usalama migodini kukabiliana na El Nino
- Sakata la mgomo wa madereva, ACT Wazalendo wataka Waziri Katambi ajiuzulu
- Mashili atimiza ahadi, akabidhi msaada wa kichomeo taka na jenereta Chuo cha Uuguzi Nzega
- Mgomo wa madereva watikisa nchini, abiria wakwama
- Rais Mwinyi : Afrika isibaki kuwa soko la teknolojia, ijenge uwezo wake wa ubunifu
- Tanzania yaendelea kujiimarisha katika usimamizi wa maafa
- Serikali yajipanga kutoa taarifa za El nino kwa wenye ulemavu
- Kilogramu 18, 078,41 za dawa za kulevya zakamatwa na DCEA katika operesheni maalum
- Watendaji wa Uchaguzi watakiwa kuzingatia viapo
- Stanbic : Maboresho ya soko la mitaji yafungua fursa mpya kwa taasisi za umma
- Makonda : Hatutaki kansa Arusha, njoo upimwe mapema
- Mlinzi afukuzwa kazi kwa tuhuma za kuwachungulia wateja wanaopata huduma wodi ya wazazi
- TARURA ichukue hatua za haraka kutatua kero ya karavati Mwanalugali, Muheza