Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama,ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kufanya tathimini ya Rushwa katika mikoa kisha kuitangaza mikoa itakayobainika kuongoza kwa vitendo hivyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama,akizungumza  wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wenye lengo la kjitathimini utendaji kazi wao kwa mwaka mzima unaoenda sambamba na uzinduzi wa Programu ya TAKUKURU rafiki yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya rushwa unaofanyika leo  Desemba 20,2022 jijini Dodoma.

Hayo ameyasema juzi jijini Dodoma wakati akifungua Mmutano mkuu wa mwaka wenye lengo la kujitathimini utendaji kazi wao kwa mwaka mzima unaoenda sambamba na uzinduzi wa Programu ya TAKUKURU rafiki yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya rushwa.

Amesema kuwa lengo la tathmini hiyo ni kupimana na kuona ni mkoa upi ambao unakiwango kikubwa cha rushwa na upi unakiwango kidogo cha rushwa kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia watendaji kujitadhimini katika maeneo yao

Amesema kuwa mapambano yao wanayapeleka katika kupambana na rushwa lakini haiwakatazi na haiwaondoi kwenye majukumu yao ya kila siku kwani majukumu waliyopewa ni ya kushughulika na kupambana na rushwa ujenzi wa maadili na stahiki kwa watumishi wa umma”

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni,akizungumza wakati wa  Mkutano Mkuu wa Mwaka wenye lengo la kjitathimini utendaji kazi wao kwa mwaka mzima unaoenda sambamba na uzinduzi wa Programu ya TAKUKURU rafiki yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya rushwa unaofanyika leo  Desemba 20,2022 jijini Dodoma.

“Nyie makamanda wangu wa Mikoa mahali pa kuanza ni kwa huyo Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Utawala na rasilimali watu akiweza huyo kufanya kazi zake vizuri mienendo na vitendo vya unadhulifu wa fedha za taifa hili letu kwenye Halmashauri zitapungua ama kuisha kabisaa kutqneni nao hawa,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salum Rashid Hamduni, amesema Tanzania ni moja ya nchi sita duniani zilizotangazwa duniani kupiga hatua katika masuala ya mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini.

Nchi nyingine zilizopiga hatua ni pamoja na Ethiopia,Sisheli,Angola,Rwanda na Senegal ambazo zimepiga hatua kutokana na utafiti uliofanywa na mashirika mbalimbali likiwemo la Transparent International.

Amesema kuwa pamoja na hayo pia wamepanda nafasi ya 87 kwa mapambano dhidi ya rushwa kati ya nchi 187 ambazo zimefanyiwa utafiti na mashirika mbalimbali.

Washiriki wa Mkutano wakimsikiliza Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wenye lengo la kjitathimini utendaji kazi wao kwa mwaka mzima unaoenda sambamba na uzinduzi wa Programu ya TAKUKURU rafiki yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya rushwa jijini Dodoma.

“Tunashukuru kufikia nafasi hiyo naimani tutaendelea kupanda zaidi nafasi za juu katika mapambano dhidi ya rushwa,”amesema.

CP.Hamduni amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa niya kila mmoja hivyo kila mtu anapaswa kumuangalia mwenzake anayehusika na vitendo dhidi ya rushwa.

Wakati huohuo CP.Hamduni akizungumzia kuhusiana na uzinduzi wa program Rafiki ya kupambana na rushwa amesema itapelekwa kila mahali mpaka kwenye kata ambapo itawasaidia wananchi kujua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao.

“Ni jukumu la kila mmoja kupambana na rushwa na si Taasisi pekee hivyo wanapaswa kutoa taarifa ambazo zinaviashiria vya rushwa,”amesema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge Wakupambana na Rushwa Afrika Tawi la Tanzania,Cecilia Pareso amesema kama Wabunge watahakikisha wanapambana na rushwa kwani ni suala la watu wote.

By Jamhuri