Wakala ya Barabara (TANROADs) Mkoa wa Dar es Salaam imetangaza kufungwa kwa Daraja la Tanzanite kwa muda wa siku 8 ili kupisha maboreshna kuweka nembo ya Tanzanite katika daraja hilo.

“TANROADS inawatangazia watumiaji wa Daraja la Tanzanite kuwa daraja litafungwa siku ya Jumatatu tarehe 2 Januari 2023 kuanzia saa 12 asubuhi na kufunguliwa siku ya Jumatatu tarehe 9 Januari 2023 saa 12 asubuhi.”

“Sababu ya kufungwa kwa daraja hili ni kwa ajili ya kuweka Nembo yaTanzanite Katika muda wote wa maboresho hayo, Daraja hili halitatumika kwa sababu za KIusalama.”

” Hivyo, Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam inawashauri watumiaji wa Daraja hilo kutumia barabara ya Kaunda na Ali Hassan Mwinyi.”

By Jamhuri