Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab (wa pili kushoto) akijumuika na Waislamu wengine kuupokea mwili wa Marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi leo kwa ajili ya swala maiti. [Picha na Ikulu] 03/03/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimpa mkono wa pole Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid mara baada ya swala ya Maiti kumswalia Marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi leo (katikati) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman Abdulla. [Picha na Ikulu] 03/03/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa tano kulia) akijumuika na  Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu kumuombea dua Mwili wa   Marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi leo  baada ya Swala ya Ijumaa.[Picha na Ikulu] 03/03/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na  Viongozi baada ya Swala ya Ijumaa na kuswalia Mwili wa   Marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi leo.[Picha na Ikulu] 03/03/2023.

By Jamhuri