Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mikoa mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya John Mwakangale wakati wa kilele cha Sherehe za Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere aliyeikabidhi kwa niaba ya Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Bw. Ahmed Salim kuhusu chakula cha Mifugo wakati alipotembelea Banda la Kampuni hiyo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya mnufaika wa Mpango wa kuwawezesha Vijana kwenye Mifugo (BBT life Mifugo) Rest Mgonja kuhusiana na Mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Bw. Ahmed Salim kuhusu ufugaji wa kisasa wa kondoo na mbuzi wa maziwa wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

By Jamhuri