Bondia wa Tanzania, Karim Mandonga, maarufu kwa jina la Mandonga Mtu Kazi, amepigwa tena na mwandondi mkongwe wa Uganda Moses Golola.

Mandonga alitolewa kwa ‘Technical Knock Out’ Jumamosi, Julai 29 katika pigano lililofanyika jijini Mwanza, Tanzania.

Watazamaji walikuwa wamejawa na msisimko walipokuwa wanamtazamaji bondia wa Tanzania ambaye amejipatia umaarufu kwenye mchezo huo, kwa bahati mbaya pigano hilo halikwenda kama alivyotarajia.

Licha ya kupambana kweli kweli, alizidiwa nguvu na Golola, ambaye hatimaye alimtoa katika raundi ya tatu, na kupata ushindi mnono kupitia Technical Knock Out.

Wiki iliyopita, Mandonga alipoteza ambano jingine dhidi ya Daniel Wanyonyi wa Kenya.

By Jamhuri